Habari zenu wanaComplex,....Ni siku nyingine nimeona Tupeane mawili matatu juu ya mambo fulani ya kimtandao ambayo huweza kurudisha nyuma sana mafanikio yetu katika maisha ya KILA SIKU.

Hivi sasa ni mitandao mingi sana imekuwa inamambo hatari na ambayo huweza kuchukua information mbali mbali kutoka kwa computer yako bila hata ya wewe kujua....Watu wanapotezwa Facebook, Twitter na nyinginezo, tatizo ni nini hasa.....Leo nimeona tuwekane sawa juu ya hili na namna ya kujilinda na HACKERS na MALICIOUS ADWARES kupitia browsers yetu kama mozzilla firefox, internet explorer, na chrome ama hata safari.

http://i.imgur.com/USg6J.jpg

Tuliowengi tunatumia mozilla, wengine wanatumia CHROME, wanaojua maana ya Internet Vulnerabilities wanatumia Safari, wanaopenda kutumia mda wao na site moja moja wanatumia Opera (sisemei kwa mobile phones) kwa ambao wanaona uvivu na kuwa na mda wa kuchezea sana wanatumia explorer....

SASA TUNAANZA
Hizi browsers hasa kwa mfano wa leo ntacheki sana na MOZILLA FIREFOX hii browser inatumiwa na wengi na ni free source, kwa ajili ya watu kushare idea za coding styles....kama wanavyosema kwenye privacy policy za mozilla lakini kumekuwa na kundi kubwa la hackers ambao wengine hawajui kama wanakuwa wanhack informations kwa manufaa gani...zaidi akomoe tu watu (black hat hacker). na wengine wanahack kwa manufaa ya kuokoa na kujenga (white hat hackers) ambao lengo lake anashow mapungufu yaliyopo kwenye systems.

ENHEE APO NDO INAKUAJE KUAJE
Kwenye mozilla leo ntaonesha vitu vichache ambavyo huweza kumfanya mtu atoe informations zake bila ya yeye kutaka....NA LEO NTADEAL na KIMOJA TU na hicho ni EXTENSIONS>>>PLUGIN

kwa upande huu wa extensions hackers huweza kutuma malicious adwares mbali mbali ambao baadae anaweza kutumia softwares hiyo kama plugin kwa browser hii na ku DECRYPT data kutoka kwa internet history, bookmarks an kuongeza toolbars ambazo wakati mwingine huwezi kujua kama kuna information zinakuwa detected.

Hapa nazungumzia watu kama keyloggers ambao wamegawanyika katika makundi zaidi ya matano japo kwa case hii ya leo ntazungumzia keyloggers wa AINA MBILI:


Kwanza kuna:
Packet analyzers:.> hawa jamaa kazi yao kubwa ni ku ENCRYPT paswords kwenye web systems kama http post: namaanisha kama web hai ENCRYPT paswords manake ni rahisi kuwa hacked hizo informations ....Tunasema hivi data zilizokuwa ENCRYPTED ni cipher text. na data ambazo hazijawa ENCRYTED (yaani decrypted) tunaziita plain text

Baada ya kumcheki huyo aina ya keylogger kuna huyu tunamuita Form grabbing based huyu jamaa kazi yake ni KUREKODI DATA ZAKO ULIZOINGIZA KWENYE FORM FULANI KWENYE WEBSITE kabla ya data zako kuwa transimitted (kuhamishiwa) kwenye database servers.

UFAFANUZI ZAIDI KWA HUYU FORM GRABBING BASED KEYLOGGER
Mfano unapojaza form ya usajili labda ya twitter or facebook ama hata emails, basi kabla ya data zako kutumwa moja kwa moja kwenda kwa database za yahoo, gmails, ama facebook basi yeye huchukua taarifa zile....na kwa namna anavyoweza kuwa katengenezwa anaweza akawa anatuma copy ya taarifa unazojaza kwa hacker huyo.

sasa zile details wakati zinapitishwa pitishwa kwa server devices kabla ya kufika kwa database ya ile website e.g mysQl ama sQl na zinginezo....Basi hacker huyu yeye anazi DECRYPT na kuzi-leak baadhi ya info zako kwa hizo devices kwa heavy softwares ambazo zinauwezo wa kudetect info za website fulan ama server fulani.

Aina nyingine ya hao KEYLOGGERS ni OPERATING SYSTEM BASED MALICIOUS yaani ni wale ambao wanachukua informations mapema sana wakati ukiwa unaTYPE kwenye keyboard yako na marangingi huwa wanatoa taarifa kwa haraka sana pindi unapogusa tu keyboard yako....hao ni kama API-based, Kernel based na Hypervisor-based

SASA PRESHA IMEPANDA EEH??? SUBIRI WANA NAMNA YA KUWAZUIA
Kwa baadhi ya hackers hutuma plugin kama software kwenye browser yako na kutaka uinstall kwa computer kama plugin kwa browser....Moja ya hizo plugin ni "PINTEREST TOOL" ambayo ni TROJAN PWS ZAQ...mfano wa mambo ambayo malware huyu kuchukua data ni hivi

http://4.bp.blogspot.com/-RrW6vgEM-X4/Ud7gB28u3dI/AAAAAAAAWng/VW1N2J3qFz4/s640/plugin_script.png


SOLUTION SASA TUNAFANYAJE:
Kwa wale ambao wanatumia AVAST VERSION 8. Hasa wenye internet security ...kazi ni ndogo sana wanachopaswa kufanya ni ku CLEAN BROWSER kutoka kwa AVAST system kama inavyoonekana hapa:Baada ya HAPO...UKO SAFE lakini kama ungependa kujihakikishia zaidi click zile browser zinazoonekana hapo kwa avast alafu RESET yaani ufte information zote ili uanze upya kama umetoka kunistall vile


JE NA SISI TUSIO NA HIYO AVAST (ANTIVIRUS) TUNAFANYAJE???
Complex hatumuachi mtu....kwa wasio na Avast watumie CCleaner software kuCLEAR informations ambazo pengine hawajui kama zimekuwa ni hatari kwa matumizi yao....Unaweza ipata CCleaner kwa forums zetu hapa hapa ama unaweza BOFYA HAPA

JE na SISI TUSIO NA HIYO AVAST INTERNET SECURITY????
Complex hatuna historia ya kuwaacha watu....Kwa wasio na hiyo avast internet security Click Hapa
Na kama uktaka ku ACTIVATE AVAST INTERNET SECURITY Cheki kwa Forums zetu hapo ipo njia ya kuactivate

Na kwa wale ambao wangependa tu wa Clean browser zao ...hawahitaji kudownload full avast internet security zaidi ku Clear hili tatizo la plugins kwa browsers zao CCLEANER PROGRAM

USHAURI WETU COMPLEX
Endapo umeingia kwenye mtandao fulani hakikisha hau-INSTALL chochote kinachoitwa PLUGIN ambazo hazieleweki kazi yake ni nini.....Moja ya Plugin za kuruhusu installation ni adobe flashplayer, adobe shockwave na zipo chache zinazojieleza wazi kazi zake muhimu

Ikitokea unaplugin umeinstall na huielew, cheki nasi kwa forums zetu post tatizo lolote na tutawekana sawa.....Kesho somo la kusecure FACEBOOK ACCOUNT ntaliweka hewani vizuri ....Santeni na msisahau kushare kwa wenzetu....Complex System Advanced Computing Skills

Like
Responses (0)
Sorry, but you are not allowed to view the replies here.
Your Reply