• Msisimko Tanzania kufuatia ushindi wa Samatta

    Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Samatta alisema: "Najivunia sana kushinda tuzo muhimu sana kiasi hiki. Naijionea fahari na kuonea fahari taifa langu pia. Natoka taifa (Tanzania) ambalo si moja ya mataifa makubwa katika soka Afrika. Kutawazwa kuwa mchezaji bora Afrika, ni jambo kubwa sana kwangu."